Mwanamke wa Australia amewaita
maafisa wa wanyama pori kumtoa nyoka wa urefu wa mita 1 mwenye sumu kali
kutoka kwenye kiatu chake.
Mnasa nyoka Rolly Burrell alimdhibiti
nyoka huyo wa rangi ya chokoleti aliyekuwa anatafuta ''joto'' nyumbani
mwa mwanamke huyo Adelaide, kusini mwa Australia.Alikuwa ametoka nje ya nyumba yake iliopo mashambani kukusanya viatu vyake na hapo akaona mkia ukipotea ndani ya kiatu chake kimoja.
Nyoka huyo ni mmoja wa wanaoonekana kuwa wenye sumu kali duniani na hupatikana katika pwani na maeneo ya ndani ya ardhi kavu Australia
"Alitoka nje kuchukua viatu vyake na akaona kitu kikitoweka kwa kasi, ALISEMA Rolly Burrel
"Aligundua kuwa ni nyoka."
Nyoka huyo ambaye ni aina inayopenda kujificha, alichiliwa msituni kando na mbali na maenoe ya makaazi ya watu .
Bwana Burrell amesema kampuni yake iliitwa kwa mara nyengine kutoa nyoka kwenye kiatu takribana mwaka mmoja uliopita.
Viatu hivyo aina ya buti, vimetengenezwa kwa ngozi ya kondoo, na hutumika sana Australia, Huwana joto zuri wakati wa msimu wa baridi, pengine ndio sababu iliomvutia nyoka huyo.
"Ndio wanaanza kuamka kutoka usingizini," Bwana Burrell anasema.
"Msimu wao wa kujamiiana umeanza kwa hivyo wanatafuta joto na wana njaa."
Comments
Post a Comment
Here