Skip to main content
Je Giggs amezea mate kuwa meneja wa Swansea?
Ryan Giggs huenda anapendelea kuwa
meneja wa klabu ya Swansea ikiwa kiongozi wa sasa Francesco Guidolin
ataachia ngazi kama tetesi zinavyobashiri.
Giggs, mwenye umri wa
42, aliihama Manchester United kama meneja msaidizi tangu July - na
kumaliza uhusiano wake wa miaka 29 na klabu hiyo.
Swansea tayari
imepata pointi 4 kutoka kwa mechi 5 walizocheza msimu huu lakini
inasemekana klabu hiyo ya Wales ina mpango wa kubadili uongozi.
Sio kwamba Giggs ndio chaguo pekee la Swansea iwapo mabadiliko hayo yatafanyika.
Isitoshe,
tangu alivyoondoka Old Trafford , Giggs amekuwa akiendeleza zaidi
biashara zake za siku nyingi kwenye maswala ya matangazo ya biashara ya
TV work na pia katika Salford City, klabu ambayo anaimiliki pamoja na
watimu wenzake wa zamani Paul Scholes, Nicky Butt, Gary na Phil.
Awali
Giggs alionesha hamu ya kumrithi Louis van Gaal kama meneja wa
Manchester United lakini naibu mwenyekiti Ed Woodward badala yake
akamchagua Jose Mourinho baada ya kumfuta kazi Louis van Gaal hapo Mei
Comments
Post a Comment
Here