Skip to main content

Posts

Showing posts from 2016

Trump: UN ni baraza la porojo

Rais mteule wa Marekani , Donald Trump, kwa mara nyengine tena amelikashifu shirika la Umoja wa Mataifa. Kupitia akauntI yake ya Twitter, amesema shirika hilo linamsikitisha kwa madai kwamba badala ya kuwa shirika lenye hadhi kuu zaidi, limekuwa kama baraza la watu kukusanyika na kupiga gumzo. Hii ni baada ya jaribio lake la kutaka kupinga azimio lililokemea mpango wa Israel kuendelea kujenga makaazi yao katika ardhi ya Wapalestina kufeli. Baraza la usalama la Umoja wa Matifa limesema kuwa Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kujenga katika ardhi ya Wapelestina. Azimiio hilo lilipitishwa Ijumaa iliyopita huku Trump akitoa onyo kwamba mambo yatakuwa tofauti wakati atakaposhika rasmi hatamu za uongozi

Madini mapya yagunduliwa Mererani, Tanzani

Madini mapya yamegunduliwa nchini Tanzania, katika eneo lenye madini ya kipekee la Manyara, na kupewa jina Merelaniite. Jina hilo limetokana na eneo ambalo madini hayo yalipatikana, Merelani (Mererani) katika milima ya Lelatema katika wilaya ya Simanjiro katika eneo la Manyara. Eneo hilo linafahamika sana kwa madini ya Tanzanite. Madini hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia ya London, chuo kikuu cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia ya Smithsonian ya Washington. Wataalamu sita waliofanya uchunguzi, kwenye makala iliyochapishwa kwenye jarida la Minerals (Madini) wanasema madini hayo yana vipande vinavyofanana na sharubu vya rangi ya kijivu vya urefu wa milimita moja hivi, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa hadi mililita 12. Kipenyo cha vipande hivyo ni mikrometa kadha. Madini hayo yanakaribiana na madini ya zoisite (aina ya tanzanite), prehnite, stilbite, cha...

Arsenal walala 2-1 mbele ya Everton

Arsenal wamepoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya Everton kutoka nyuma na kuondoka na ushindi wa 2-1. Washika bunduki hao walishinda michezo mitatu mfululizo walianza vyema katika mchezo dhidi ya Everton baada ya Alexis Sanchez kupiga safi mkwaju wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari uliombabatiza mlinzi Ashley Williams na kuingia wavuni. Everton walisawazisha na kuwa dakika chache kabla ya kwenda mapumzikoni baada ya Seamus Coleman kumalizia vyema mpira uliopigwa na mlinzi Leighton Baines. Msimamo wa ligi ya EPL 2016/17 Kipindi cha pili kila timu ilirejea kwa lengo la kuchukua alama tatu lakini ni Everton ndio waliofanikiwa baada ya Williams kufuta makosa yake kwa kuifungia Everton goli la pili na la ushindi. Nahodha wa timu ya Everton Phil Jagielka alitolewa kwa kadi nyekundu dakika chache tu kabla ya kumalizika kwa mchezo huo baada kupata kadi ya pili ya njano. Kwa matokeo hayo Arsenal wanabaki nafasi ya pili wakiwa na alama 34...

Lionel Messi akutana na kijana aliyevalia jezi ya karatasi Afghanistan

  Mvulana kutoka nchini Afghanistan aliyepata umaarufu sana mtandaoni alipopigwa picha akiwa amevalia karatasi kama jezi ya Lionel Messi mechi amefanikiwa kukutana na shujaa huyo wake. Picha ya Murtaza Ahmadi, mwenye miaka sita, akiwa amevalia karatasi hiyo iliyoandika nambari ya jezi ya Messi pamoja na jina lake ilivuma sana mwezi Januari mtandaoni. Mwishowe, alipokea jezi halisi kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona, ambayo pia ilikuwa imetiwa saini na mchezjai huyo. Sasa, wawili hao wamekutana ana kwa ana mjini Doha, kwa mujibu wa kamati andalizi ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar. Mvulana wa Afghanistan apewa jezi ya Messi Kiatu cha Lionel Messi chawakera raia wa Misri Barcelona wamo nchini Qatar kucheza mechi ya kirafiki na Al Ahli Jumanne. Ahmadi anatarajiwa kutembea kuingia uwanjani akiandamana na Messi. "Ni picha ambayo ulimwengu ulitaka kuona," aliandika mkuu wa kamati hiyo Jumanne. "Mvulana wa miaka sita akikutana na shujaa wake, #Messi...

Nyoka atafuta' joto' kwenye kiatu Australia

Mwanamke wa Australia amewaita maafisa wa wanyama pori kumtoa nyoka wa urefu wa mita 1 mwenye sumu kali kutoka kwenye kiatu chake. Mnasa nyoka Rolly Burrell alimdhibiti nyoka huyo wa rangi ya chokoleti aliyekuwa anatafuta ''joto'' nyumbani mwa mwanamke huyo Adelaide, kusini mwa Australia. Alikuwa ametoka nje ya nyumba yake iliopo mashambani kukusanya viatu vyake na hapo akaona mkia ukipotea ndani ya kiatu chake kimoja. Nyoka huyo ni mmoja wa wanaoonekana kuwa wenye sumu kali duniani na hupatikana katika pwani na maeneo ya ndani ya ardhi kavu Australia "Alitoka nje kuchukua viatu vyake na akaona kitu kikitoweka kwa kasi, ALISEMA Rolly Burrel "Aligundua kuwa ni nyoka." Nyoka huyo ambaye ni aina inayopenda kujificha, alichiliwa msituni kando na mbali na maenoe ya makaazi ya watu . Bwana Burrell amesema kampuni yake iliitwa kwa mara nyengine kutoa nyoka kwenye kiatu takribana mwaka mmoja uliopita. Viatu hivyo aina ya buti, vimetengenezwa kwa...

Je Giggs amezea mate kuwa meneja wa Swansea?

Ryan Giggs huenda anapendelea kuwa meneja wa klabu ya Swansea ikiwa kiongozi wa sasa Francesco Guidolin ataachia ngazi kama tetesi zinavyobashiri. Giggs, mwenye umri wa 42, aliihama Manchester United kama meneja msaidizi tangu July - na kumaliza uhusiano wake wa miaka 29 na klabu hiyo. Swansea tayari imepata pointi 4 kutoka kwa mechi 5 walizocheza msimu huu lakini inasemekana klabu hiyo ya Wales ina mpango wa kubadili uongozi. Sio kwamba Giggs ndio chaguo pekee la Swansea iwapo mabadiliko hayo yatafanyika. Isitoshe, tangu alivyoondoka Old Trafford , Giggs amekuwa akiendeleza zaidi biashara zake za siku nyingi kwenye maswala ya matangazo ya biashara ya TV work na pia katika Salford City, klabu ambayo anaimiliki pamoja na watimu wenzake wa zamani Paul Scholes, Nicky Butt, Gary na Phil. Awali Giggs alionesha hamu ya kumrithi Louis van Gaal kama meneja wa Manchester United lakini naibu mwenyekiti Ed Woodward badala yake akamchagua Jose Mourinho baada ...

Mtoto apandikizwa pua mpya India

Madaktari nchini India wamepandikiza pua mpya katika uso wa mvulana wa miaka 12 iliokuwa imemea katika paa lake la uso. Pua ya Arun Patel iliharibika alipougua ugonjwa wa homa ya kichomi Maambukizi hayo yaliharibu pua yake akiwa mtoto mdogo. Upandikizaji kama huo ulifanywa nchini China mwaka 2013 ambapo mtu mmoja ambaye aliharibu pua yake katika ajali alipewa pua mpya. Wazazi wa Arun walimchukua na kumpeleka katika daktari mwengine katika kijiji cha jimbo la kati la Madhya Pradesh ambapo aliugua kichomi mda mfupi baada ya kuzaliwa. Lakini matibabu aliyopewa yaliongeza hali yake na hivyobasi kupoteza pua yake. Miaka kadhaa baadaye,kundi moja la madaktari katika mji wa Indore liliamua kufanya upasuaji usiokuwa wa kawaida ambapo Arun alipata pua mpya

Leicester yamsajili mshambuliaji wa Nigeria

Klabu ya Leicester City imemsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow kwa kandarasi ya miaka 4 itakayogharimu pauni milioni 16. Southampton,Everton na West Ham walikuwa wakitafuta saini ya mchezaji huyo. Musa ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Leicester baada ya kipa Ron-Robert Zieler ,beki Luis Hernandez na kiungo wa kati Nampalys Mendy. Mchezaji huyo alijiunga na CSKA mwaka 2012 na kufunga mabao 54 kati ya mechi 168 alizocheza,na amefunga mabao 11 katika mechi 58 alizochezea Nigeria tangu aanze kucheza mwaka 2010.

Mamba 100 watoroka hifadhi katika mafuriko

Mamlaka nchini Uchina inajaribu kutafuta takriban mamba 100 waliotoroka kutoka kwenye hifadhi moja baada ya mafuriko makubwa yanayoshuhudiwa nchini humo. Mafuriko hayo yaliwawezesha mamba hao kuogelea na kuondoka kwenye eneo lilizingirwa kwenye hifadhi hiyo katika mkoa wa Anhui. Ni nadra sana kupata Mamba hao wa Uchina mwituni. Hata hivyo mamba huwindwa kutokana na ngozi yao inayouzwa kwa bei ghali mno pamoja na nyama yao na pia hutumika kuwaburudisha watalii. Takriban watu 180 wamekufa maji kutokana na mafuriko hayo makubwa yanayoendelea kushuhudiwa nchini China. Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kutorokea maeneo yenye milima ilikutoroka mafuriko yanayochacha

Mamia kupigwa picha za utupu Uingereza

Mamia ya watu watavua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherehekea utamaduni katika mji wa Hull, Uingereza. Tukio hilo litakuwa la kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni. Washiriki watapakwa rangi ya samawati Jumamosi na kisha wapigwe picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull. Mradi huo unatekelezwa na mpiga picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art Gallery. Picha zitakazopigwa zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja. Tunick, anayetoka New York, amewahi kufanya kazi kama hiyo kwingine. Amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico City na mjini Munich nchini Ujerumani Germany. Bw Tunick amesema kazi zake “hugusia historia ndefu ya Sanaa ya utupu”. "Mavazi ni Sanaa ya mtu mwingine,” anasema. “Fashoni ni Sanaa. Kwa kuondoa hilo (mavazi), nitakuwa nafanya kazi...

Ashtakiwa kumtusi Magufuli katika WhatsApp

Raia mmoja wa Tanzania amefunguliwa mashtaka kutokana na ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo anadaiwa kumtusi Rais John Pombe Magufuli. Mulokozi Kyaruzi ameshtakiwa chini sheria uhalifu wa mtandaoni. Ni mtu wa pili kushtakiwa chini ya sheria hiyo kwa tuhuma za kumtusi rais. Sheria hiyo ilikosolewa sana kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza wakati ilipoanza kutekelezwa mwaka uliopta. Kyaruzi anadaiwa kuandika: "'Kwani rais Magufuli hana washauri? hashauriki? Ama ni mjinga tu? Ni Mpumbavu sana. Haangalii sheria iliopo kabla ya kufungua mdomo ama anaugua ugonjwa wa Mnyika''?

Msichana asiye na mikono ashinda tuzo ya muandiko bora.

    Msichana wa miaka saba aliyezaliwa bila mikono ameshinda shindano la muandiko mzuri nchini Marekani. Anaya Ellick kutoka Chesapeake,Virginia hatumii viungo vya kumsaidia wakati anapoandika. Wakati anapoandika yeye husimama huku akishikilia kalamu yake katika mikono. Mwalimu wake mkuu Tracy Cox kutoka shule ya Greenbrier Christian amemtaja kuwa mtu wa mfano mwema. ''Yeye uhakikisha kuwa hakuna kitu kinachomzuia kufanya atakalo'',alisema Cox.''Ni mkakamavu na ana muandiko mzuri katika darasa lake''. Msichana huyo anadaiwa kuwashinda washindani wengine 50 ili kushinda taji hilo la kitaifa. Orodha hiyo ya tuzo huwazawadi wanafunzi wenye akili, matatizo ya kimwili, au ulemavu endelevu.