kijana akiwa kwenye usaili wa kazi Kupata kazi ya ndoto zako si jambo jepesi, na inawezekana ikawa ni vigumu zaidi kama hujui waajiri wanataka nini kutoka kwako. Ulimwengu wa wa ajira - kwa kampuni kubwa na ndogo - unabadilika kwa kasi sana. Lakini kuna eneo moja ambalo ni la muhimu kuzingatiwa kwa kila msaka ajira: usaili wa ana kwa ana. "Usaili huo ni sehemu kubwa zaidi ya mchakato wa ajira," amesema Jane Tippin, ambaye ni gwiji wa masuala ya rasilimali watu ambaye hutumiwa na kampuni kubwa ya benki nchini Uingereza ya Lloyds Bi Tippin anaamini kuwa uwezo wako wa kujibu maswali mbele ya mtu ama jopo la watu linaweza kujenga ama kubomoa mustakabali wako wa kupata ajira. Hivyo, unahitajika kujiandaa kikamilifu kabla ya kuingia kwenye chumba cha usaili wa ana kwa ana. Zifuatazo ni dondoo muhimu zitakazokusaidia kufaualu usaili huo: 1. Fanya utafiti. ...
BLESSED TO BLESS OTHERS