Haki miliki ya picha AFP Image caption Hotuba ya wazi inayofahamika kutoka kwa Rais Bouteflika ilikua mwaka 2014 Kwa raia wengi wa Algeria ni vigumu kuelewa ni kwa vipi rais wao mwenye miaka 82 ,aliyeugua kiharusi miaka sita iliyopita na kupata shida kwenye kutembea au kuzungumza anaweza kuongoza nchi. Hakuna aliyeamini ilipotangazwa kuwa Abdelaziz Bouteflika anawania awamu ya tano mwezi Aprili-hata mwenyewe hakujitokeza binafsi siku ya Jumapili kujisajili kuwania nafasi hiyo . Waalimu, wanafunzi, wanasheria hata waandishi wa habari waliingia mitaani kuandamana wakiwa na hasira , walionekana kutokubaliana na hatua ya kuongozwa na mtu ambaye haonekani. Wengi wanahofu kuwa kutopatikana kwa mrithi wa Rais Bouteflika, ambaye aliingia madarakani mwaka 1999, kunaweza kusababisha hali ya usalama kuyumba nchini humo. Kiongozi wa kwenye TV Kwa mara ya mwisho alionekana akihutubia Umma mwaka 2014 -hotuba ya shukrani kwa raia wa Algeria kwa kuuamini utawala wake baaa ya kushinda uchagu...
BLESSED TO BLESS OTHERS