Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2017

Puerto Rico yapiga kura kujiunga na Marekani

Himaya ya Marekani ya Puerto Rico imepiga kura ya kuomba bunge la Congress kuifanya kuwa jimbo la 51 la Marekani. Zaidi ya asilimia 97 ya wapiga kura walipendelea kujiunga na Marekani badala ya kuwa huru au kuwa himaya tu ya kujisimia. Hata hivyo asilimia 23 ya wapiga kura walijitokeza kupiga kura licha ya upinzani kususia kura hiyo. Marekani kumsaka mtoto wa Osama Hata hivyo uamuzi wa mwisho hauko mikononi mwao bali kwa Congress. Kura hiyo ya maoni ya mwaka 2017 ilitishwa na serikali baada ya kushuhudiwa kwa hali ngumu ya kiuchumi ambayo wengi wanadai kuwa imetokana na hali ya sasa ya Puerto Rico ambayo ni nusu kati ya kuwa na uhuru au himaya linalojisimamia.

Mkuu wa mashtaka afutwa kwa kukataa kupokea simu ya Trump

Aliyekukuwa mwendesha mashtaka wa cheo cha juu mjini New York, amefichua kwa alifutwa kazi na Rais Donald Trump baada ya kupokea simu kadha zisizokuwa za kawaida kutoka kw rais huyo wa Marekani. Preet Bharara aliambia shirika la ABC wiki hii kuwa alihisi simu hizo kutoka kwa Rais Trump zilikuwa zimevuka mipaka ya kawaida inayotenganisha ofisi ya rais na uchunguzi huru wa uhalifu. Bwan Bharara alisema kuwa alifutwa baada ya kukataa kuchukua simu ya tatu ya Trump. Ikulu ya white House haikujibu mara moja madai hayoiya bwana Bharara. Trump: Nitamteua mkurugenzi mpya wa FBI haraka iwezekanavyo Rais Trump achukizwa na tuhuma za Comey James Comey anadaiwa kukataa kumtii rais Trump Bw Bharara ambaye aliteuliwa na Obama na kuhudumu eneo la Manhattan, alisema ilionekana kuwa Trumo alijaribui kujenga uhusiano fulani baada ya wawili hao kukutana mwaka 2016. "Rais obama hakunipigia simu hata mara moja katika kipindi cha miaka saba unusu," Bw Bharara alisema.

MAYAI NA UMUHIMU WAKE

Kula yai kwa siku kunaweza kuwasaidia watoto wadogo wenye utapiamlo kuongeza urefu kulingana na utafiti wa miezi sita huko Ecuador. Haijalishi ikiwa ni yale yaliyo chemshwa, au ya kukaanga, na watafiti wanasema ni njia isiyo ghali ya kuzuia kudumaa. Miaka miwili ya kwanza maishani ni ya muhimu sana kwa ukuaji na maendeleo na kudumaa kunaweza kuleta madhara makubwa. Lishe duni ni sababu kubwa ya kudumaa, pamoja na maambukizi ya utotoni na magonjwa. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, watoto milioni 155 chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa (wafupi kwa umri wao). Wengi wao wanaishi katika nchi zilizo na mapato ya chini na ya kati na wataalamu wa afya wamekuwa wakitafuta njia za kukabiliana na suala hilo. Lora Iannotti na wenzake walifanya majaribio katika nyanda za vijijini ya Ecuador na kuwapa watoto wadogo sana (wenye umri wa miezi sita hadi tisa) mayai, ili kuona kama yataweza kuwasaidia. Nusu tu kati ya watoto 160 ambao walishiriki katika majaribio wali...

UMUHIMU WA NDOA

Utafiti nchini Uingereza umebaini kwamba ndoa inaleta afya ya moyo. Utafiti uliofanywa kwa zaidi ya miaka 13 kwa zaidi ya watu laki tisa ambao wana matatizo aina tatu ya moyo, umebaini kwamba wanandoa wenye kiwango kikubwa cha lehemu wana asilimia 16 ya kuishi kuliko wale ambao hawako kwenye ndoa. Wale anaougua maradhi ya kisukari na presha pia walikuwa katika hali nzuri. Watafiti wanaamini, ingawa hawawez

Tanzania yapoteza matrilioni ya pesa kupitia usafirishaji mchanga wa madin

Tanzania imepoteza takriban shilingi za kitanzania trilioni 188 (dola milioni 84 za Marekani ) katika kipindi cha miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba. Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi March mwaka huu na Rais John Magufuli. Ripoti hii imekuja siku chache baada ya Ripoti ya kwanza iliyojikita kueleza kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na usafirishaji wa mchanga wenye madini. Ripoti ya Madini:Rais Magufuli amshauri Waziri ajiuzulu Rais Magufuli amfuta kazi katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Tanzania Kamati hii ya sasa iliundwa na wataalam wa masuala ya uchumi na wanasheria ambao walikuwa na jukumu la kutazama mikataba ya madini na athari za kiuchumi kwa Tanzania. Katika Ripoti ya Jumatatu, Tume imedai kuwa Kampuni ya madini yenye makazi yake nchini Canada, Acacia ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya madini haikuwahi kusajiliwa nchini humo, hivyo imekuwa ikif...

VYUO VIKUU BORA DUNIANI

  1 Massachusetts Institute of Technology (MIT) 2 Stanford University 3 Harvard University 4 California Institute of Technology (Caltech) 5 University of Cambridge 6 University of Oxford 7 UCL (University College London) 8 Imperial College London 9 University of Chicago 10 ETH Zurich - Swiss Federal Institute of Technology 11 Nanyang Technological University, Singapore (NTU) 12 Ecole Polytechnique Fédérale de Lausanne (EPFL) 13 Princeton University 14 Cornell University 15 National University of Singapore (NUS) 16 Yale University 17 Johns Hopkins University 18 Columbia University 19 University of Pennsylvania 20 The Australian National University =21 Duke University =21 University of Michigan =23 King's College London =23 The University of Edinburgh 25 Tsinghua University 26 The University of Hong Kong 27 University of California, Berkeley (UCB) =28 Northwestern University =28 The University of Tokyo 30 The Hong Kong Univ...

Vyuo vikuu bora zaidi duniani mwaka 2017

Orodha mpya ya kila mwaka ya vyuo vikuu bora zaidi duniani imetangazwa, ambapo chuo kikuu cha Massachusetts Institute of Technology (MIT) cha Marekani bado kinaongoza. Vyuo vikuu vya Stanford na Harvard - pia kutoka Marekani - kadhalika vimeendelea kushikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia. Orodha hiyo ilishirikisha vyuo vikuu karibu 1,000. Facebook kuwa somo chuo kikuu India Vyuo vikuu hupimwa kwa mambo kama vile majarida na vitabu vya kisomi vilivyochapishwa, makala zilizonukuliwa, maoni ya wasomi pamoja na waajiri na pia ushiriki wa vyuo vikuu hivyo katika ngazi ya kimataifa. Chuo kikuu cha Nairobi kimeorodheshwa kuwa kati ya nambari 801 na nambari 1000, kutoka kuanzia nambari 701 hadi 1000mwaka jana, sawa na Chuo Kikuu cha Makerere. Vyuo vikuu 10 bora zaidi duniani kwa mujibu wa QS World University Rankings l College London Massachusetts Institute of Technology (MIT) Stanford Harvard California Institute of Technology (Caltech) Cambridge Oxford Univ...

Mabaki ya binadamu 'wa kwanza' yapatikana Morocco

Uchunguzi umebainisha kuwa dhana ya kuwa asili ya binadamu wa kwanza ni kutoka Afrika ya Mashariki zaidi ya miaka laki mbili iliyopita sio kweli. Visukuku vya binadamu watano wa mapema imepatikana Kaskazini mwa Afrika na inaonyesha binadamu wa kwanza aliishi miaka 100,000 zaidi ya vile ilivyodhaniwa. Prof Jean-Jacques Hublin, kutoka Leipzig, Ujerumani, anasema kuwa ugunduzi huu unaweza "kuandika upya vitabu vya kiada" kuhusu kuibuka kwetu . "Sio hadithi ya hayo kutokea kwa njia ya haraka katika 'shamba la Edeni' mahali fulani barani Afrika. Ilikuwa ni maendeleo ya taratibu. Kwa hiyo kama kulikuwa na bustani ya Edeni, ilikuwa ni kote kote Afrika. " Mji wa kale sana wagunduliwa Misri Binadamu wa kale huenda 'hawakuishi zamani sana' Prof Hublin alikuwa akiongea katika mkutano wa wanahabari katika chuo kimoja mjini Paris, ambako aliwaonyesha waandishi kisukuku ambacho timu yake ilichimbua katika eneo la Jebel Irhoud, Morocco. Sampu...