Beyonce amefichua nyimbo zilizomo kwenye albamu yake mpya itakayoambatana na filamu mpya The Lion King remake na albamu hiyo imejumuisha wasanii nyota na wa juu wa muziki kutoka Afrika. Wasanii wa Nigeria Tiwa Savage na Mr Eazi wanatumbuzia katika wimbo wa 'Keys to the Kingdom', wengine Tekno na Yemi Alade katika kibao 'Don't Jealous Me'. Burna Boy ana kibao cha kipekee au solo, 'Ja Ara E', huku msanii wa Cameroon Salatiel akionekana akiimba na Beyonce na Pharrell Williams katika kibao 'Water'. Wasanii wengine wa Afrika ni pamoja na Wizkid wa Nigeria, Shatta Wale wa Ghana, na Busiswa na Moonchild Sanelly kutoka Afrika kusini. Alipotangaza mpango huo kwa mara aya kwanza wiki iliyopita, Beyonce alisema "Ilikuwa ni muhimu kuwa muziki usiimbwe na wasanii nyota na wenye vipaji bali iandaliwe na waandaaji wa Kiafrika. Ubora na moyo (mapenzi) vilikuwa vitu muhimu kwangu. "Ni mchanganyiko...
BLESSED TO BLESS OTHERS