Ni kitu cha kwanza wengi wetu tunakitazama asubuhi na kitu cha mwisho kukiangalia usiku.Simu zetu haziko mbali nasi na tunaziangalia kila baada ya dakika 12, kwa mujibu wa mamlaka ya kudhibiti mawasiliano nchini Uingereza, Ofcom. Ni mahusiano ambayo yanaonekana kuwa yatadumu zaidi, hivyo tunakudokeza sheria tano za matumizi ya simu ambayo yanapaswa kutazamwa kwa umakini. 1. Kuzungumza na simu wakati wa kula chakula Watu wengi hufanya hivyo, na zaidi ya 26% ya vijana wanakubali suala hili ''Simu zinapaswa kuwa zimezimwa saa zote wakati wa chakula, mikutano na sherehe,''anasisitiza Diana Mather, mshauri wa masuala ya tabia. ''Mtu uliyenaye ni mtu aliye muhimu zaidi.Hakuna miongoni mwetu asiye na umuhimu. Hata kutazama televisheni inakuwa imezimwa kwa baadhi ya watu wakati mkiwa kwenye meza ya chakula Zaidi ya watu wanne kati ya watano walio na umri wa miaka 55 na zaidi wanafikiri haikubaliki kutazama ujumbe wa simu ukilinganisha na 46% ya umri wa...
BLESSED TO BLESS OTHERS