Skip to main content

Mwana wa Osama bin Laden asakwa na Marekani

Mwana wa Osama bin Laden aorodheshwa na Marekani miongoni mwa magaid wanaosakwa na MarekaniMarekani imesema kuwa imemuorodhesha mwana wa mwisho wa Osama Bin Laden, Hamza, katika orodha ya magaidi wanaosakwa na taifa hilo.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa Hamza Bin Laden ameanza kushiriki katika maswala ya kundi la al Qaeda, kundi la jihad lililofadhiliwa na babake.
Amesema kuwa atalipiza kisasi mauaji ya babake yaliotekelezwa na kikosi maalum cha Marekani kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya Wamarekani.
Sasa atapigwa marufuku kwa kufanya biashara na raia wa Marekani huku mali yake ikipigwa tanji.
Mamake Hamza ni Khairiah Sabar, mmoja wa wake za Osama aliyekamatwa wakati wa shambulio la wanajeshi wa Marekani kwenye maficho ya Osama mjini Abbotabad nchini Pakistan mwaka 2011.
Mkuu wa kitengo cha usalama cha kundi la al-Qaeda Ibrahim al-Banna pia ameongezwa katika orodha hiyo .
Marekani imetoa kitita cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayemkamata al-Banna.
Hamza bin Laden alitambuliwa kuwa mmoja wa viongozi wa al-Qaeda mwaka 2015 na baadaye akaapa kulipiza kisasi mauaji ya babake mwezi Julai mwaka uliopita
Katika ujumbe wa sauti wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama," (Sote ni Osama), na uliochapishwa katika mitandao, aliapa lazima angelipiza kisasi mauaji ya babake mwaka 2011 nchini Pakistan.
''Tutaendelea kuwasaka na kuwapiga popote pale mtakapokuwa mumejificha ati nyuma ya pazia za usalama kwa maovu munayoyaendeleza ,Palestina, Afghanistan, Syria, Iraq, Yemen, Somalia na kote kwenye ardhi ya waislamu mnayokalia,'' shirika la habari la Reuters lilimnukuu.
''Na kwa wale wanaodhania kuwa tutakuwa tukilipiza kisasi mauaji ya Osma ole wenu, kwanini sisi tutakuwa tukilinda dinia ya kiislamu'' alisema Hamza.
Hamza, kulingana na wachanganuzi, alitambulishwa na kiongozi wa kidini wa kundi la al-Qaeda Ayman al-Zawahiri katika ujumbe huo uliolenga kuwavutia vijana ambao kwa sasa wamejiunga kwa wingi na kundi la Islam

Comments

Popular posts from this blog

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...

Wafungwa wa Guantanamo Bay wawasili Saudi Arabia

Kundi la wafungwa wa Yemen waliozuiliwa nchini Marekani katika Gereza la Guantanamo Bay wamewasili nchini Saudi Arabia. Waandishi kutoka katika shirika la habari la AFP wamesema watu watatu wameonekana wakipokelewa na familia zao katika uwanja wa ndege ambao kwa kawaida hupokea viongozi Mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh. Kuhamishwa kwa wafungwa kumetokea siku mbili baada ya Ikulu ya Marekani kuahidi kuendelea na mpango wake wa kuhamisha wafungwa kutoka kataka Gereza la Guantanamo Bay, wakipinga suala ambalo limekuwa likipingwa vikali na Rais mteule wa Marekani Donald Trump.