Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2017

Mwana wa Osama bin Laden asakwa na Marekani

Marekani imesema kuwa imemuorodhesha mwana wa mwisho wa Osama Bin Laden, Hamza, katika orodha ya magaidi wanaosakwa na taifa hilo. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa Hamza Bin Laden ameanza kushiriki katika maswala ya kundi la al Qaeda, kundi la jihad lililofadhiliwa na babake. Amesema kuwa atalipiza kisasi mauaji ya babake yaliotekelezwa na kikosi maalum cha Marekani kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya Wamarekani. Osama aliacha dola milioni 29 kufadhili Jihad Mzozo kuhusu shamba la Osama Pakistan Sasa atapigwa marufuku kwa kufanya biashara na raia wa Marekani huku mali yake ikipigwa tanji. Mamake Hamza ni Khairiah Sabar, mmoja wa wake za Osama aliyekamatwa wakati wa shambulio la wanajeshi wa Marekani kwenye maficho ya Osama mjini Abbotabad nchini Pakistan mwaka 2011. Mkuu wa kitengo cha usalama cha kundi la al-Qaeda Ibrahim al-Banna pia ameongezwa katika orodha hiyo . Marekani imetoa kitita cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayemkamata al-Banna. ...

Wafungwa wa Guantanamo Bay wawasili Saudi Arabia

Kundi la wafungwa wa Yemen waliozuiliwa nchini Marekani katika Gereza la Guantanamo Bay wamewasili nchini Saudi Arabia. Waandishi kutoka katika shirika la habari la AFP wamesema watu watatu wameonekana wakipokelewa na familia zao katika uwanja wa ndege ambao kwa kawaida hupokea viongozi Mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh. Kuhamishwa kwa wafungwa kumetokea siku mbili baada ya Ikulu ya Marekani kuahidi kuendelea na mpango wake wa kuhamisha wafungwa kutoka kataka Gereza la Guantanamo Bay, wakipinga suala ambalo limekuwa likipingwa vikali na Rais mteule wa Marekani Donald Trump.

Wanadiplomasia wa Urusi waliofurushwa Marekani waondoka

Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kuwa wanadiplomasia 35 wa Urusi waliofurushwa na rais Barack Obama kutoka Marekani wameondoka wakiandamana na familia zao . Urusi ilituma ndege maalum ya kuwarudisha nyumbani. Wanadiplomasia hao waliamuriwa kuondoka Marekani baada ya Urusi kushtumiwa kuwa ilijaribu kuingilia uchaguzi wa hivi majuzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa mitandaoni. Vyombo vya kijasusi vya Marekani vinadai kuwa utawala wa Urusi ndio ulioamuru kudukuliwa kwa hasa tovuti ya chama cha Democratic ili kuvuruga kapeni za bi Clinton na kumsaidia Donald Trump ambae sasa ndiye rais mteule.

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Rubani apatikana mlevi kabla ya ndege kuondoka

Polisi huko Canada wamemkamata rubani mmoja aliyepatikana ,ndani ya ndege ya abiria kwenye chumba cha marubani akiwa amelewa chakari kwa mujibu wa vipimo alivyofanyiwa. Rubani huyo alikuwa amepangiwa kuendesha ndege hiyo kwa safari ya kutoka uwanja wa ndege wa Calgary Canada hadi nchini Mexico ndipo lakini wafanyikazi wenzake wakamuona hakuwa katika hali sawa na kupiga ripoti. Kisha punde baadae akaanguka na kuzirai. Sasa amezindukia mashtaka ya kutaka kuendesha ndege akiwa mlevi na utovu wa nidhamu kazini. Baadae rubani mwengine aliendesha ndege hiyo ya shirika liitwalo Sunwing iliyokuwa inaelekea Cancun mjini Mexico, ikiwa na abiria zaidi ya 100.

Sony yamuomba radhi Britney Spears baada ya ''kumuua'

Kampuni ya muziki ya Sony imemuomba radhi mwanamuziki nyota wa pop Britney Spears, baada ya ukurasa wake rasmi kutangaza kuwa amefariki. Kampuni hiyo ya burudani iliondoa mara moja ujumbe wake batili, ikisema kuwa akaunti yake ilikuwa "imedukuliwa" lakini kwamba hali hiyo "imerekebishwa. Sony iliongeza kusema kuwa '' samahani kwa Britney Spears na mashabiki wake kwa mkanganyiko wowote uliojitokeza". Britney Spears mwenye umri wa miaka 35 hakujibu moja kwa moja kupitia mtandao wake wa Twitter, lakini meneja wake amethibitisha kuwa muimbaji huyo yuko ''salama salmini''. Hali kadhalika Ukurasa wa Twitter rasmi wa afisa wa Sony Bob Dylan pia ulionekana kudukuliwa. Ulitumwa ujumbe uliosema: "pumzika kwa amani @britneyspears" katika muda sawa na ule uliotumwa ujumbe bandia wa Sony.

Ishara ya Hollywood yabadilishwa kuwa ''Hollyweed

Raia wa Los Angeles ambao ndio majirani wa eneo la kuigiza filamu maarufu 'Hollywood' waliamka mwaka mpya na kuona kwamba ubao wa ishara ya eneo hilo maarufu umebadilishwa na kuwa 'Hollyweed'. Vyombo vya habari katika eneo hilo vimeripoti kwamba maafisa wanalichukulia swala hilo kuwa dogo na kwamba wanaendelea na uchunguzi. Ishara hiyo ilioko katika mlima Lee ina herufi zenye urefu wa futi 45. Wapiga kura mjini California waliidhinisha sheria ya kuhalalisha bangi katika kura iliofanyika wakati mmoja na uchaguzi wa Marekani mnamo tarehe 8 Novemba. Mzaha huo hatahivyo haujaharibu herufi za ishara hiyo kwa kuwa herufi 'O' zilifanywa na kuwa 'E.' Gazeti la Los Angeles Times limeripoti kwamba mtu mmoja alirekodiwa akipanda katika ishara hiyo ili kubadilisha herufi hizo. Mzaha kama huo ulifanyika mnamo mwaka 1976 ili kulegeza sheria dhidi ya bangi.