Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2016

Trump: UN ni baraza la porojo

Rais mteule wa Marekani , Donald Trump, kwa mara nyengine tena amelikashifu shirika la Umoja wa Mataifa. Kupitia akauntI yake ya Twitter, amesema shirika hilo linamsikitisha kwa madai kwamba badala ya kuwa shirika lenye hadhi kuu zaidi, limekuwa kama baraza la watu kukusanyika na kupiga gumzo. Hii ni baada ya jaribio lake la kutaka kupinga azimio lililokemea mpango wa Israel kuendelea kujenga makaazi yao katika ardhi ya Wapalestina kufeli. Baraza la usalama la Umoja wa Matifa limesema kuwa Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kujenga katika ardhi ya Wapelestina. Azimiio hilo lilipitishwa Ijumaa iliyopita huku Trump akitoa onyo kwamba mambo yatakuwa tofauti wakati atakaposhika rasmi hatamu za uongozi

Madini mapya yagunduliwa Mererani, Tanzani

Madini mapya yamegunduliwa nchini Tanzania, katika eneo lenye madini ya kipekee la Manyara, na kupewa jina Merelaniite. Jina hilo limetokana na eneo ambalo madini hayo yalipatikana, Merelani (Mererani) katika milima ya Lelatema katika wilaya ya Simanjiro katika eneo la Manyara. Eneo hilo linafahamika sana kwa madini ya Tanzanite. Madini hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia ya London, chuo kikuu cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia ya Smithsonian ya Washington. Wataalamu sita waliofanya uchunguzi, kwenye makala iliyochapishwa kwenye jarida la Minerals (Madini) wanasema madini hayo yana vipande vinavyofanana na sharubu vya rangi ya kijivu vya urefu wa milimita moja hivi, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa hadi mililita 12. Kipenyo cha vipande hivyo ni mikrometa kadha. Madini hayo yanakaribiana na madini ya zoisite (aina ya tanzanite), prehnite, stilbite, cha...

Arsenal walala 2-1 mbele ya Everton

Arsenal wamepoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya Everton kutoka nyuma na kuondoka na ushindi wa 2-1. Washika bunduki hao walishinda michezo mitatu mfululizo walianza vyema katika mchezo dhidi ya Everton baada ya Alexis Sanchez kupiga safi mkwaju wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari uliombabatiza mlinzi Ashley Williams na kuingia wavuni. Everton walisawazisha na kuwa dakika chache kabla ya kwenda mapumzikoni baada ya Seamus Coleman kumalizia vyema mpira uliopigwa na mlinzi Leighton Baines. Msimamo wa ligi ya EPL 2016/17 Kipindi cha pili kila timu ilirejea kwa lengo la kuchukua alama tatu lakini ni Everton ndio waliofanikiwa baada ya Williams kufuta makosa yake kwa kuifungia Everton goli la pili na la ushindi. Nahodha wa timu ya Everton Phil Jagielka alitolewa kwa kadi nyekundu dakika chache tu kabla ya kumalizika kwa mchezo huo baada kupata kadi ya pili ya njano. Kwa matokeo hayo Arsenal wanabaki nafasi ya pili wakiwa na alama 34...

Lionel Messi akutana na kijana aliyevalia jezi ya karatasi Afghanistan

  Mvulana kutoka nchini Afghanistan aliyepata umaarufu sana mtandaoni alipopigwa picha akiwa amevalia karatasi kama jezi ya Lionel Messi mechi amefanikiwa kukutana na shujaa huyo wake. Picha ya Murtaza Ahmadi, mwenye miaka sita, akiwa amevalia karatasi hiyo iliyoandika nambari ya jezi ya Messi pamoja na jina lake ilivuma sana mwezi Januari mtandaoni. Mwishowe, alipokea jezi halisi kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona, ambayo pia ilikuwa imetiwa saini na mchezjai huyo. Sasa, wawili hao wamekutana ana kwa ana mjini Doha, kwa mujibu wa kamati andalizi ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar. Mvulana wa Afghanistan apewa jezi ya Messi Kiatu cha Lionel Messi chawakera raia wa Misri Barcelona wamo nchini Qatar kucheza mechi ya kirafiki na Al Ahli Jumanne. Ahmadi anatarajiwa kutembea kuingia uwanjani akiandamana na Messi. "Ni picha ambayo ulimwengu ulitaka kuona," aliandika mkuu wa kamati hiyo Jumanne. "Mvulana wa miaka sita akikutana na shujaa wake, #Messi...