Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2020

Fahamu ukweli wa dhana tano kuu kuhusu nyoka na maadhimisho ya nyoka duniani

Huku Tarehe 16 mwezi Juni ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya nyoka duniani mnyama huyo hutazamwa kwa hatari kubwa, waerevu na mara nyingine hata kuhusishwa na imani potofu na uchawi katika baadhi ya jamii za Kiafrika. Kwa kawaida nyoka anakuwa juu ya orodha ya mambo ambayo mtu anaogopa maishani mwake. Maelfu ya watu duniani hufariki kutokana na sumu kali ya nyoka baada ya kuumwa kila mwaka kwa mujibu wa shirika la afya duniani. Ukosefu wa matibabu na hata matibabu mabaya hufanya vifo hivyo kutokingika. Uso kwa uso na nyoka hatari Nyoka mwenye macho matatu agunduliwa Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika Nigeria Sumu ya nyoka ni dawa ya kumaliza uchungu Kuumwa na nyoka huenda kusionekane kuwa janga baya la kiafya. Lakini katika maeneo mengine duniani ni hatari kila siku na huenda kukasababisha maafa ama hata kubadilisha maisha ya mtu. Pengine ndio sababu ya kuwepo dhana tofuati, baadhi potofu, kuhusu wanyama hawa. Hebu tuwafahamu zaidi. CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES ...