China itakuwa na gwaride kubwa la kijeshi hapo kesho kwa ajili ya kusheherekea miaka 70 ya chama kinachotawala nchini humo cha 'Communist' , na nchi hiyo imehaidi kuonyesha silaha mpya zinazotengenezwa nchini humo katika mji wa Beijing.
Je, ni silaha gani watakazozionyesha na kwanini China sasa inatambuliwa kama taifa la pili lenye bajeti kubwa ya kijeshi duniani?
Oktoba mosi kuna mipango gani?
Gwaride la kijeshi ni miongoni mwa mambo makubwa yatakayofanyika katika sherehe hiyo kubwa itakayofanyika katika eneo la Tiananmen litahudhuriwa na maafisa wakubwa, wananchi kadhaa walioallikwa na askari 188 kutoka nchi 97.
Msemaji wa waziri wa ulinzi alisema hivi karibuni kuwa China haina mpango au haiitaji kuonyesha nguvu iliyonayo lakini wamelenga kuonyesha upendo, amani na namna China inawajibika.
Gwaride hili limelenga kuwavutia wengi na litatumika kuonyesha vitu.
Wizara ya uinzi imeripoti kuwa wanajeshi 15,000 watashiriki pamoja na 59 ambao watatoka vikosi mbalimbali , huku silaha 580 zitaonyeshwa katika mitaa mbalimbali na ndege za kijeshi 160 zitarushwa angani.
Rais Xi Jinping atakagua gwaride hilo katika makutano ya Chang'an mjini Beijing na baada ya hapo ndege za jeshi zitaruka katika eneo la Tiananmen.
Kwa mara ya kwanza, askari 8,000 kutoka China ambao walikuwa mashujaa wa ulinzi wa amani wa Umoja wa mataifa wataweza kushiriki.
Ni Silaha gani tutaziona?
Jeshi la 'People's Liberation Army (PLA)' lina shauku ya kuonyesha silaha mpya katika hadhara ambazo zimeshaanza kutumika.
Miongoni mwa silaha ambazo zinatarajiwa kuoneshwa:
- Silaha mpya ya DF-41 ambayo wachambuzi wanasema kuwa imelenga kutumika sehemu yoyote ulimwenguni itaweza kuonyeshwa.
- Silaha nyingine ni MIRV ambayo ina muongozo maalumu wa ufanyaji kazi, ina uwezo wa kupiga maeneo 10 tofauti katika eneo kubwa .
- Mashine nyingine ni DF-17, inatajwa kuwa gari kubwa lenye uwezo wa kubeba mzigo mkubwa na ina kasi kubwa.
- Silaha nyingine mpya za magari, ndege na meli za kijeshi zitaweza kuonyeshwa.
- Two unmanned aircraft Ndege mbili za kijeshi ambazo hazikutajwa majina zikiwa na muundo wa ndege isiyokuwa na rubani pia zitaonyeshwa ingawa zinalengwa kuitwa DR-8 .
- Y-20 ni ndege ya kijeshi ambayo ina uwezo wa kutoa angalizo kwa watumiaji
H6-N ni aina mpya ya bomu nchini China ambayo ina uwezo wa kufanya milipuko kadhaa angani.
PLA imesisitiza kuwa itaonyesha uvumbuzi waote mpya uliofanyika nchini humo katika sekta ya ulinzi na namna maboresho walioyafanya.
Ni gharama gani inatumika katika jeshi la China?
Gharama inayotumika katika jeshi la China inazidi kuongezeka tangu rais wa nchi hiyo kutangaza kufanya maboresh mwaka 2015.
Zaidi ya muongo, bajeti ya wizara ya ulinzi imeongezeka kwa asilimia 10 kila mwaka na sasa bajeti hiyo kufikia dola $168.2bn hivyo kufanya taifa hilo kuwa la pili duniani.
China ina uwekezaji mkubwa zaidi wa ulinzi barani Asia mwaka 2018 kwa kutumia $56.1bn kwa silaha na utafiti wa usalama na maendeleo, ambapo ni sawa na zaidi ya asilimia 33 ya bajeti ya ulinzi nchini China.
Matokea ya hivi karibuni ya matumizi na sababu ya matumizi hayo imeandikwa katika wizara hiyo.
Kwa msisitizo wa idara hiyo ya usalama, matumizi ya China yamefananishwa na matumizi ya Marekani ambayo bado iko juu kwa jumla ya bilioni $643.3b kwa mwaka 2018.
Pamoja na kwamba China ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani lakini wizara ya ulinzi ilitumia robo ya kile kilichotumika Marekani mwaka 2017, na imefanya kazi kwa $100 kwa kila mtu ambayo sawa na 5% ya Marekani.
China inafikiria kutumia vipi jeshi lake?
China inasema kuwa mpango wake wa kutengeneza jeshi lenye nguvu ni kutaka kuendelea kuwa katika vigezo vya kimataifa na kuongoza kuwa na jeshi linaloongoza duniani .
China imeweza kutengeneza kisiwa huko kusini mwa China mwishoni mwa mwezi june kwa ajili ya jeshi.
Eneo hilo limetengeza mfumo wa (A2AD) linaaminiwa kuwa lina uwezo wa kuzuia Marekani kuingia kusini mwa China kutokea ufukweni mwa bahari.
Je, China inakaribia kuipita Marekani?
Moja ya tofauti kubwa ambayo itaonekana hapo kesho katika gwaride la maadhimisho haya na ya mwaka 2015, ni sherehe za angani.
Ikiwa China inaadhimisha miaka 70 ya ushindi kati yao na Japan katika vita ya pili ya dunia.
Gwaride linaangazia kusheherekea mafanikio ambayo China yameyapata katika upande wa uvumbuzi na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.
Taifa hilo linataka kuwa na jeshi kubwa la kisasa zaidi duniani kwa mwaka 2035 na jeshi bora zaidi ifikapo mwaka 2049.
Pamoja na matarajio yote mazuri, yanahitaji uwekezaji mkubwa zaidi.
China inahitajika kuboresha malipo ya wanajeshi, kuwa na mafunzo mambo ambayo yatagharimu pakubwa.
Comments
Post a Comment
Here